Mkuu wa wilaya ya ubungo Mhe. Kheri Denice James amewataka watumishi wa Manispaa ya Ubungo kufanya kazi kwa ushirikiano, ueledi na ubunifu mkubwa katika kutekeleza majukumu yao ili kuongeza ufanisi wa kazi na ubora wa utoaji wa huduma kwa wananchi wa manispaa hiyo.
Hayo ameyazungumza leo juni 22, 2021 wakati alipotembelea ofisi za manispaa hiyo kwa lengo la kuongea na wakuu wa idara na vitengo ikiwa ni hatua ya kujitambulisha na kutoa muelekeo wa namna ya kufanya kazi kwa ushirikiano pamoja na kuzingatia kanuni, sheria, taratibu, miongozo na maelekezo ya viongozi yasiyo kinyume cha sheria.
Katika kikao hicho, mhe. Mkuu wa Wilaya amewapongeza watumishi wa manispaa hiyo kwa utekelezaji mzuri wa shughuli za maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo usafi, elimu, afya pamoja na uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia 10% ya fedha za mapato ya ndani.
“Niko kwenye Halmashauri inayofanya vizuri kwenye sekta mbalimbali ikiwemo usafi, barabara zetu ni safi nawapongeza sana; nimekuja kuungana nanyi tushirikiane” ameeleza James.
Aidha, James amewasisitiza watendaji wa manispaa hiyo kuwa wabunifu katika kutekeleza shughuli zao ikiwemo namna bora ya utoaji wa mikopo isiyo na riba kwa vikundi vya wananwake, vijana na watu wenye ulemavu ili kuzalisha ajira nyingi kwa vijana pamoja na kukuza uchumi wa wananchi.
“Ninapenda tufanye kazi kama timu na iwe timu yenye matokea sio maneno, nawaahidi ushirikiano wakati wote, tuchape kazi”
Akiongea kwa niaba ya Wakuu wa Idara na Vitengo, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Beatrice Dominic amemshukuru mheshimiwa Mkuu wa Wilaya kwa kuwatembelea na kuongea nao na ameahidi kutoa ushirikiano pamoja na kutekeleza maelekezo yote aliyosema.
Mhe. Mkuu wa wilaya Kheri Device James aliapishwa jana tarehe 21 june, 2021 katika halfa ya kuapisha Wakuu wa Wilaya wapya wa Mkoa wa Dar Es Salaam iliyofanyika katika ukumbi wa anatoglo uliopo Mnazi mmoja jijini humo.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa