DC UBUNGO AKABIDHI HUNDI YA MILLIONI 804 KWA WAJASIRIAMALI WADOGO Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mheshimiwa Kheri James amekabidhi hundi ya milioni 804,720,000 kwa wajasiriamali wadogo ambao wanastahili kupata fedha hizo zilizotokana na asilimia 10 ya mapato yake ya ndani.
Fedha hizo zimenufaisha Wajasiriamali 918 kwa vikundi 118 ambapo vikundi vya vijana 30, wanawake 81 na watu wenye ulemavu 7 kwa ajili ya kwenda kukuza biashara zao.
Akikabidhi hundi hiyo kwa vikundi amesisitiza kila mmoja anayeenda kupata mikopo hiyo kwenda kukuza uchumi na kuwawezesha kufikia malengo.
Serikali ina lengo la kuwasaidia wananchi wake na kwa kuangalia hilo Manispaa ya Ubungo imetenga fedha kwaajili ya kikundi cha vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.
"Kila mmoja akachape kazi ilikuweza kupata faida kutokana na mikopo hii na mkatumie fedha hizo kwa biashara mlizokusudia awali". Aliendelea kueleza Kheri.
Kheri alisistiza kwa Viongozi kuepukana na migogoro kwenye vikundi na kuendelea kushirikiana kwa pamoja.
Aidha, aliendelea kwa kusema kuwa ukimuwezesha mwanamke umeisaidia jamii nzima wakiwemo watoto na hata akina baba.
Mikopo hii inaenda kuwawezesha walemavu pia watakwenda kuimarisha uchumi wao kwa kuanzisha biashara zao kujikimu na familia zao.
"Ni jukumu la kila mmoja wetu atakae pata mkopo huu leo akakuze uchumi wake kwa kuhakikisha wanaenda kuzalisha na mwishowe bidhaa zote tunazofuata kariakoo, alisema Kheri.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa