- Leo Disemba 08, 2022 Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri James akiwa ameambatana na Kamati yake ya Ulinzi na Usalama (KUU) pamoja na wataalamu kutoka Manispaa ya Ubungo wameendelea na ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa miradi ya afya
- Kwa siku ya leo miradi ya afya iliyotembelewa ni miradi 10 ambayo jumla ina thamani ya shilingi Bilioni 2.7 ambapo miradi hiyo inajengwa katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Ubungo
- Akiongea katika ziara hiyo Mhe. Kheri James ameipongeza idara ya afya na wakandarasi ambao wanasimamia miradi hiyo kwa kazi kubwa ambayo wanaifanya ambayo inaenda kutafsiri dhamira ya dhati ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye kugatua huduma ya afya kwa wananchi
- Pamoja na pongezi hizo Mkuu wa wilaya pamoja na kamati ya Ulinzi na usalama wameainisha baadhi ya mapungufu ambayo wamebaini katika ziara hiyo ikiwemo miradi kadhaa kuwa nyuma ya muda kuelekea kwenye kukabidhi miradi hiyo. Vituo vya afya vya Palestina, Makuburi, Temboni pamoja na Msingwa ni miongoni mwa miradi ambayo kasi yake hairidhishi na tayari mkuu wa wilaya ametoa maelekezo ya kufanya kazi kwa masaa 24 ili kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati. Kwa kuongezea hilo mkuu wa wilaya amesema mpaka kufikia Disemba 25 vituo hivyo viwe vimekamilika kwa asilimia 100
- Katika mradi wa Hospitali ya Wilaya, Kamati imeridhishwa na kasi ya ujenzi unaoendelea ambapo kituo hicho kitakapokamilika kitakua kinatoa huduma za kibingwa kwa magonjwa ya kina mama pamoja na kina baba. Akiongea katika ziara hiyo mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Dkt. Imani Mwelang'ombe amesema kuwa anamshukuru mhe. Rais kwa kuendelea kuleta fedha za ujenzi wa kituo hicho ambapo itasaidia kusogeza karibu huduma kwa wananchi
- Nae kaimu mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Dkt. Peter Nsanya ametoa shukrani nyingi kwa mkuu wa Wilaya pamoja na kamati ya Ulinzi na Usalama kwa kutenga muda kufanikisha ziara hii muhimu ya ukaguzi wa miradi ya afya ambayo ni muhimu sana kwa wananchi
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa