Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kisare Makori tarehe 20/7/2020 amemkabidhi Bi. Nyangoma James Bajaji aliyomuomba Mhe. Rais siku ya tarehe 19/6/2020 eneo la Ubungo katika makao makuu ya Wilaya hiyo yaliyopo Luguruni.
Wakati wa makabidhiano hayo mkuu wa wilaya alimsisitiza Bi.Nyangoma kuhakikisha anaitumia bajaji hiyo vizuri na kufanya kazi ipasavyo ili imsaidie kiuchumi
Kaitunze bajaji hii na yenyewe ikutunze ikakuongezee kipato cha kuisaidia familia yako na watoto wako" alisisitiza Makori.
"Nimshukuru Mhe.Rais kwani ni kiongozi anayejali wanyonge na aendelee na moyo huo huo kwani umesaidia wananchi wengi kupata maendeleo na hata taifa zima". Alisisitiza Mkuu wa Wilaya.
Vile vile Mkuu wa Wilaya alisema kuwa uongozi wa Wilaya umeshiriki ipasavyo katika ununuzi na kuhakikisha kuwa Bajaji hiyo ina vibali vyote kama Bima na Sumatra.
Mwisho Bi.Nyangoma alimshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kumkabidhi bajaji hiyo na kutoa shukrani zake kwa Mhe.Raisi kwa kumsaidia kupata bajaji itakayomsaidia kujipatia kipato kitakachosaidia familia yake.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa