Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe.Kisare Makori tarehe 14/8/2020 atembelea eneo la soko la Shekilango na mbezi ilikujionea changamoto ambazo wafanyabiashara wa maeneo hayo wamekuwa wakilalamika na kuzitolea ufumbuzi changamoto zao.
Wakati akitembelea maeneo hayo aliongozana na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Ndg.James Mkumbo, Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic na wataalam kutoka katika Manispaa hiyo.
Dhumuni la kutembelea katika masoko hayo ni kutatua changamoto na kuhakikisha wafanyabiashara wanakuwa katika mazingira ya amani wanapokuwa wanafanyabiashara zao.
Nitolee ufafanuzi wa eneo hili la soko la shekilango liko chini ya umiliki wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kuanzia leo ijulikane hivyo. alisema Makori
Aidha Dc aliagiza uchaguzi ufanyike wa kuchagua viongozi wapya wa soko la shekilango na kufikia jumatatu uchaguzi uwe umefanyika ili soko lipate uongozi mpya kwani muda wa ukomo wa viongozi wa masoko ni mwaka mmoja tu kwa mujibu wa sheria za uendeshaji wa Manispaa pamoja na sheria ndogo za uendeshaji wa masoko.
Pia Dc aliongeza kuwa muda wa kudumu madarakani ni mwaka mmoja ila uongozi wa soko uliopo sasa una zaidi ya mwaka mmoja kwa hiyo kuna kila sababu ya kufanya uchaguzi.
Vilevile makubaliano ya tozo za malipo yaliyopitishwa kwa mabanda ya soko hili la shekilango ni elfu sabini na tano kwa mabanda ya mbele, elfu hamsini kwa mabanda yaliyo katikati na elfu ishirini na tano kwa mabanda ya nyuma.
Aidha niagize TAKUKURU kufanya uchunguzi katika suala zima la akaunti ya saccos ya soko la shekilango kutokana na ukaguzi uliofanyika kuonyesha kuna ubadhilifu usio wa haki. Aliongeza Dc
Ikiwemo hati ya mashaka ya saccos hiyo, udanganyifu wa taarifa za fedha na kutokuitishwa kwa mkutano mkuu wa chama n.k
Sambamba na hayo kwa wafanya biashara wa Mbezi Dc alisema kuwa "tunawajengea mabanda matano yenye thamani ya Milioni mianne na tisini na sabakwa ajili yenu.
Pia hakutakuwa na ulipaji wa kodi zaidi ya ushuru na kila mfanyabiashara kuhakikisha anakitambulisho cha mjasiriamali.
Mwisho Dc aliwataka wafanyabiashara kufanyabiashara kwa amani baada ya changamoto zao kutatatuliwa na kukubaliana na maagizo yaliyotolewa.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa