Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kisare ametoa ufafanuzi juu ya mgogoro wa shamba lililopo eneo la Goba Kisauke linalolamikiwa na familia ya Mziwanda kuwa wamenyang'anywa na Manispaa ya Ubungo
Akitoa ufafanuzi huo leo mbele ya waandishi wa habari na wananchi wa eneo la Kisauke mtaa wa kulangwa kata ya Goba, Kisare ameeleza kuwa mgogoro wa shamba hilo upo katika hatua za utatuzi ambapo mpaka sasa familia ya Mziwanda haina nyaraka za kuthibisha umiliki wa eneo hilo hali iliyopelekea Manispaa kuwa ndio msimamizi wa shamba hilo kwa mujibu wa sheria.
"Nimeona nitoe ufafanuzi juu ya mgogoro huu ili kujenga uelewa wa namna mgogoro huu ulivyoanza na hatua za utatuzi wake lakini pia kuondoa dhana kuwa familia ya Mziwanda wananyang'anywa eneo lao kinguvu"
Aidha, Kisare ameagiza kufunga nyumba zotezilizopo eneo hilo pamoja na kutofanya muendelezo wowote katika eneo hilo ikiwemo ujenzi na uuzwazi viwanja katika shamba hilo na atakayekiuka sheria zitachukuliwa dhidi yake.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa