Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri James Leo tarehe 22/06/2022 ametoa maelekezo yafuatayo kwa watendaji na viongozi
1. USAFI NA MAZINGIRA;
■DC amewataka watendaji wa Kata na Mitaa kuhakikisha usafi unaimarika kwenye maeneo yao ikiwa ni pamoja na kusimamia maeneo ambayo machinga wameondolewa na kuwaondoa wanaorudi ili mji uwe safi
■Ametoa siku Tatu kwa watendaji wa kata zilizopo Tarafa ya kibamba na Idara ya Mazingira kuhakikisha wanasimamia usafi kwenye maeneo yao kwani ni machafu.
Aidha, DC amezipongeza kata za tarafa ya Magomeni kwa kusimamia vyema uondoaji wa machinga kwenye maeneo yao.
• ULINZI NA USALAMA;
■James amewataka viongozi hao kuhakikisha mitaa yote inakuwa na vikundi vya ulinzi shirikishi, kuondoa kamluni ya QNET kwenye mitaa yao kwa kuhakikisha wenye nyumba wote ambao wamepangisha kampuni hiyo wanawaondowa,
■Ili kulinda maadili ya katika jamii DC amewataka watendaji na Wenyeviti kuhakikisha vigodoro na ngoma zinazovunja maadili zisichezwe kwenye maeneo yao.
• ANWANI ZA MAKAZI;
■Ili kufanikisha zoezi la Sensa ya watu ba makazi linalotarajiwa kufanyika mwezi Agosti,
DC amewataka watendaji na Wenyeviti kuhakikisha hadi kufikia tarehe 17 Julai,2022 zoezi la uwekaji wa vibao liwe limefikia 100% kwani asilimi 58% ni ndogo.
■Aidha, James ameipongeza kata ya Sinza kwa kuwa Kata ya kwanza Kiwilaya kufanikiwa zoezi hilo na ku kuelekeza viongozi wa kata hiyo Mtendaji Kata na Mhe. Diwani na Mwenyekiti wa Mtaa wa Sinza C ambae amekuwa wa kwanza kumaliza zoezi hilo wapatiwe motisha kwa kazi Nzuri waliyoifanya.
■Kwa wazabuni ambao wanalega kutekeleza jukumu hilo DC ameelekeza wachukuliwe hatua.
• USHIRIKISHWAJI WA WANANCHI;
■DC amewataka viongozi hao kuhakikisha wananchi wanashirikishwa kwenye ajenda zote za maendeleo ya maeneo yao ikiwa ni pamoja na kuwajulisha fedha zote za miradi zinavyoingia na namna fedha hizo zinatumika.
■Aidha ametoa shukrani kwa Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa Kuleta kidato cha tano na sita katika shule ya Sekondari ya Mashujaa iliyopo Sinza na Kiluvya iliyopo Kibamba na amewataka viongozi hao kulipokea swala hilo kwa Kierkegaard mikakati bora kwa wanafunzi watakaopangiwa shule hizo.
Baadhi ya Wenyeviti na Watendaji kata na Mitaa wanasikiliza maelekezo yanayotolewa na Mkuu wa wilaya ya ubungo Mhe. Kheri james kwenye kikao kazi kilichofanyika tarehe 22 Mei, 2022
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa