Manispaa ya Ubungo kwa mwaka wa fedha mpya wa 2020/2021 imetoa mikopo isiyo na riba yenye thamani ya shilingi Millioni 567,440,000 kwa wajasiriamali 1086 kwenye vikundi 90 vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu kwa lengo la kuwakwamu kutoka kwenye wimbi la utegemezi na kufikia malengo
Mikopo hiyo imetolewa Leo tarehe 11 august 2021 ambapo vikundi hivyo vilipewa semina namna ya kuendesha biashara zao pamoja na namna watakavyopata pesa hizo ambazo shilingi 295,000,000.00 kutoka kwenye mfuko wa wanawake zitagaiwa kwa vikundi 56 , Tsh 221,790,000 kutoka kwenye mfuko wa vijana zitagaiwa kwa vikundi 27, na Tsh 50, 550,000 kutoka kwenye mfuko wa walemavu zitagaiwa kwa vikundi 7
Akiongea wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyoanza Jana Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri James amewasisitiza wanufaika kuhakikisha wanafanya marejesho ya pesa za Serikali na kuhakikisha wanaweka malengo na pesa hizo watakazo pata pamoja na uaminifu
"Wakina mama changamkieni Fursa hii, mkafanye maendeleo, mkaingize kipato na Serikali inaendelea kuwajali na kuwathamini, mkatumie pesa hizi ipasavyo. Alisema kheri
Alikadhalika Afisa Maendeleo Manispaa ya Ubungo Rose Mpeleta Aliewaeleza wanufaika wa mikopo kuwa lengo la mikopo hiyo inayotolewa na Halmashauri ni nikumkwamua Mwanamke,kijana na watu wenye ulemavu kutoka kwenye wimbi la utegemezi ili waweze kufikie malengo yao
"Mfanye marejesho ili muweze kunufaika zaidi na zaidi, mikopo hii ni ya wote unapofanya marejesho na mwingine anaweze kukopa" alielezea Mpeleta
"Msichukue mkopo mkaenda kununua vijora, mhakikishe mnafanya mambo ya maendeleo ili muweze kufanya marejesho na kuweza kukopa tena" Alisisitiza Mpeleta
Nae Michael Charles mnufaika wa mikopo hiyo inayotolewa na Halmashauri ameshukuru kwa Serikali kuweza kuwajali na kuahidi kuhakikisha kikundi chao kuwa mstari wa mbele kufanya marejesho
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa