- Leo Novemba 10, 2022 Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri James amefanya kikao kazi kati ya wenyeviti wa serikali za mitaa na Mameneja wa DAWASA Wilaya ya Ubungo ili kufanya tathmini ya changamoto ya maji iliyopo sasa pamoja na kuweka mikakati ya kumaliza changamoto hiyo kwa Wilaya ya Ubungo
- Katika kikao hicho James amesema kuhusu tatizo la maji linaloikumba Dar es Salaam kwa sasa ni lazima kwanza kukubali kuwa tatizo lipo kisha kuendelea kutekeleza mikakati ya kumaliza tatizo hilo ambalo limesababishwa na kupungua kwa kina cha maji katika mto Ruvu.
- Kwasasa serikali imekuja na mpango wa kuchimba na kufufua visima vya maji ambavyo vitaongeza maji kwenye mfumo mzima wa DAWASA na kupelekea ahueni kwa wananchi
- Wakiongea katika kikao hicho baadhi ya wenyeviti wa Serikali za mitaa wamesema kuwa DAWASA ihakikishe inatekeleza ratiba ya mgao walioweka na kama kutakua na mabadiliko ya ratiba hiyo kuwe na taarifa mapema ili wananchi waelewe
- Aidha kwa upande mwingine James amempongeza Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa mikakati aliyoelekeza kukabiliana na tatizo hili la maji ikiwemo mpango wa kufufua visima kale na kuchimba visima vipya ambapo siku ya kesho Rais Samia anatarajiwa kukabidhi mitambo kwaajili ya kuchimba visima hivyo katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Ubungo na Dar es Salaam kwa ujumla
"Mhe. Rais anafanya kazi kubwa sana kukabiliana na tatizo la maji kwa Dar es salaam nzima. Wenyeviti muwe wa kwanza kutambua na kumtia moyo Mhe. Rais kwa kazi nzuri na kubwa anayoifanya" Alisema
- Wakati kikao hicho kikiendelea, Mhe. Mkuu wa wilaya alifanya mawasiliano kwa njia ya simu na Waziri wa Maji Mhe. Juma Aweso ambapo amewaondoa hofu wenyeviti hao kuhusu tatizo la maji ambalo juhudi zinaendelea kufanyika kupunguza adha hiyo. Aweso pia amewapongeza mameneja wa DAWASA kwa wilaya ya Ubungo kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya kukabiliana na changamoto hii.
- Akijibu hoja za Wenyeviti Meneja wa DAWASA Kibamba ndugu Elizabeth Sankere amesema kuwa hoja zote wamezichukua na wameahidi kuzifanyia kazi haraka sana kutoka sasa. Kwa upande mwingine Sankere amewapongeza wenyeviti hao kwa kutoa ushirikiano kwa DAWASA
@dawasatz
#ubungoyetufahariyetu
#dawasa
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa