Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mheshimiwa Kheri James mapema leo amefungua kampeni ya chanjo ya Polio itakayofanyika kwa muda wa siku 4 kuanzia Leo tarehe 18 Mei,2022 Hadi tarehe 21 Mei,2022 katika Kituo Cha Afya Cha amani kilichopo kata ya kwembe
Akifungua kampeni hiyo Kheri amesisitiza wazazi kupeleka watoto wao kupata chanjo hiyo kwani ni bora na salama kwa watoto walio chini ya miaka mitano ili kuwakinga
"Tunasisitiza watoto wapate chanjo hii kwani mtoto asipopata CHANJO inapelekea kupata ugonjwa wa kupooza na mwisho hupelekea kifo " alieleza kheri
Aidha Mganga mkuu Manispaa ya Ubungo Dkt.Peter Nsanya ameendelea kuwaomba wazazi kufika katika Vituo vya afya na wilaya ya Ubungo tayari imeshafika katika Vituo vyote,
Aliendelea kusema kuwa ni fursa kwenu kuweza kufika na kuwapatia watoto chanjo hiyo salama
Mmoja wa wazazi aliyepeleka mtoto wake kupata chanjo Bi.happiness ameshukuru Manispaa ya Ubungo kuwawezesha kuwekea chanjo katika Vituo vilivyokaribu na makazi yao na kuwasisitiza wazazi wenzie kujitokeza kwa wingi kuwapeleka watoto wao kupata chanjo
Nb. "Polio ni ugonjwa hatari, tuwakinge watoto wetu
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa