Kamati ya ushauri ya Wilaya(DCC) imepitisha Makisio bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 ya shilingi Billioni 109,449,392,100 kwaajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, fedha za ruzuku ya mishahara na matumizi mengineyo
Baraza hilo ambalo limehudhuriwa viongozi vyama vya siasa mbalimbali vikiongozwa na Chama Cha Mapinduzi CCM, limefanyika leo tarehe 13/2/2023 ambapo Mkuu wa Wilaya Mhe.Hashimu Komba Alisisitiza katika bajeti hiyo vipaumbele ambavyo vinatakiwa kuangaliwa na kuzingatiwa ni kuongeza ukusanyaji wa mapato, kuboresha miundombinu ya barabara, elimu na afya pamoja na kuboresha mkakati wa utoaji taarifa za Maendeleo
Aidha, Komba alipongeza kwa mwaka wa fedha 2021/2022 halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imeweza kukusanya vizuri mapato mpaka kufikia 103%
wajumbe wa baraza la kamati ya ushauri ya wilaya wakichangia mawazo mbalimbali yenye lengo la kuboresha na kuweka maslahi mazuri kwa wana ubungo
Komba aliendelea kwa kusema kuwa mpaka sasa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa mwaka wa fedha 2022 - 2023 imefikia asilimia 51 ya makusanyo kwa robo mbili ambapo imevuka kiwango cha asilimia 50 kufikia mwezi Disemba 31, 2022
Aidha wajumbe walipendekeza swala la ukusanyaji wa mapato liweze kusimamiwa vizuri na kusisimamia vyanzo vya makusanyo sambamba na mikopo ya asilimia 10 ambayo hutolewa kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ambayo haijarejeshwa walengwa waweze kusimamiwa na kufuatiliwa waweze kurejesha
Nae Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ndugu Amos Maziku wakati akichangia amesema, rasilimali kubwa ya Manispaa ya Ubungo ni watu wake hivyo ameshauri kuandaliwa kwa mipango madhubuti ya kuendelea kujenga uwezo kwa wananchi ili kuongeza tija ya uzalishaji mali kwenye shughuli zao za kila siku
Katika Majumuisho ya kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Hashim Komba ameyapokea mapendekezo yote kwa ahadi ya kuyatekeleza kwa maslahi mapana ya wananchi wa Ubungo
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa