Diwani wa kata ya Sinza maanispaa ya Ubungo Rahael Nyange Awino amezindua rasmi Kamati mpya ya hospitali ya Sinza parestina na kuitaka ifanye kazi yake Kwa ufanisi ili kuboresha huduma za afya katika hospitali hiyo.
Awino, amezindua Kamati hiyo leo Machi 4, 2022 baada ya Kamati iliyopita kumaliza muda wake, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa lapazi uliopo lugulini na kuhidhuliwa na mganga Mkuu wa Manispaa hiyo.
Amesema, Kamati ya ushauri ya hospitali ni chombo mhimu Sana katika uendeshaji wa huduma za hospitali na ndio kiunganishi kikubwa cha wananchi na Serikali yao ngazi ya hospitali katika utoaji wa huduma
Kazi yenu ni ya uwakilishi Kwa wananchi Kwa kusikiliza kero zao na kuziwasilisha Kwa wataalamu Kwa ajili ya utatuzi, wananchi wanatamani kupata huduma bora na ninyi ndio mtatimiza hitaji Lao Kwa kupunguza malalamiko Yao"
Awino, ameendelea kisistiza kuwa Kamati hiyo lazima ibuni mfumo mzuri wa kushughulikia malalamiko kabla hayajafika ngazi za juu ikiwemo changamoto ya upatikanaji wa Sawa, nidhamu ya watumishi na utoaji wa huduma sahihi Kwa gharama wanazozimudu.
"Kamati hii inawawakilisha wananchi katika kufanya maamuzi juu ya utoaji wa huduma katika hospitali, Kamati ni look cha menejimenti ya hospitali inatumia kupata mrejesho wa namna wanavyotoa huduma zamatibabu Kwa wananchi tukatimize julumu Hilo mhimu.
Katika kuthibitishwa nafasi Yao ya uwakilishi Kwa jamii, wanakamati wameahidi kufanyika daraja nzuri Kati ya Serikali na wananchi Kwa kuhakikisha hospitali inatoa huduma Bora
Aidha, wanakamati wameahidi kuhamasisha jamii wajiunge na bima ya afya ili wananchi wawe na uhakika wa kupata huduma wakati wote bila shida yoyote.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa