Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (TAMISEMI) Mhe. Festo Dugange, anayeshughulikia Afya amewaagiza waganga wafawidhi wa vituo vya kutolea huduma za afya kuongeza Kasi ya ukusanyaji wa mapato ili kupunguza utegemezi wa kifedha kutoka Serikali kuu Kwa ajili ya kununua dawa, vifaa tiba na vitendanishi.
Naibu waziri ametoa maelekezo hayo Novemba 24,2021 wakati alipofanya ziara ya kikazi ya kujionea utoaji wa huduma kwenye kituo cha afya Sinza na kufuatia malalamiko ya wananchi juu ya utoaji wa huduma usioridhisha.
Dugange amesema Kwa upande wa afya Serikali imejipanga kuhakikisha upatikanaji huduma bora unakuwa Kwa kiwango cha juu ikiwemo Uwepo wa dawa za kutosha vituoni
Kutokana na umuhimu huo, Dugange amekielekeza kituo cha afya Sinza kuhakikisha ifikapo tarehe 30 mwezi desemba, 2021 kituo kiwe na uwezo wa kukusanya milioni 5 Kwa siku badala ya milioni 3 Hadi 4.5 inayokusanywa kwa sasa.
Aidha, amewataka watumishi kufanya kazi Kwa kuzingatia maadili ikiwemo kutojihusisha na vitendo vya rushwa na kuwa na lugha mbaya kwa wateja badala yake watumie lugha nzuri Kwa wagonjwa
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa