Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mtoto Manispaa ya Ubungo imepanga kutoa elimu kwa jamii namna ya kudhibiti na kukomesha matukio ya unyanyasaji kwa wanawake na watoto ili kuwa na jamii yenye ustawi.
Mkakati huo umeelezwa leo Oktoba 21, 2022 kwenye kikao cha kujadili taarifa za utekelezaji wa kamati hiyo kwa kipindi cha robo ya kwanza ambapo watoto wameonekana kuwa wahanga wa vitendo vya unyanyasaji hasa wa kingono.
Suala la lishe pia ni jambo la msingi katika kuangalia ulinzi na usalama wa mtoto, hivyo kamati imeshauri shule ziwe na somo la mapishi kwa videndo ili watoto waweze kujipikia pale wazazi au walezi wanapokuwa kwenye majukumu mengine.
Ili familia ziwe na uhakika wa chakula hasa kwa wanawake wajane, wanawake wameshauriwa kujishughulisha na biashara ndogondogo ili kuwa na usalama wa chakula katika familia badala ya kuwa ombaomba au kusubiri msaada hali inayopelekea lishe duni hasa kwa watoto na wajawazito.
Akieleza utekelezaji wa shughuli za kamati hiyo Afisa Ustawi wa jamii Manispaa hiyo ndugu Zainabu Masilamba ameeleza kuwa, katika kipindi cha julai hadi septemba 2022 matukio ya ukatili yameonekana kukithiri kwenye kata za Mabibo, Kimara, Ubungo, Saranga, Goba, Makuburi, Mburahati na Makurumla
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa