Taasisi ya Friends Of Samia, Leo Februari 14 siku ya Wapendanao duniani (Valentine's day) imeitumia siku hii kutoa zawadi mbalimbali kwa wazazi na wamama wajawazito katika hospitali ya Palestina iliyopo Sinza Manispaa ya Ubungo
Taasisi hiyo imefanya zoezi hilo wakiongozwa na balozi wao msanii wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole ambapo wametoa zawadi zao kupitia vifurushi mbalimbali
Akiongea katika hafla hiyo kaimu mganga mkuu wa hospitali hiyo dokta Nchang'wa Nhumba ameishukuru sana taasisi ya Friends of Samia kwa zawadi zao kwa wagonjwa na ametumia nafasi hiyo kuwaomba watu na taasisi zingine kuiga mfano huo
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa