Hafla fupi ya uchangiaji kwa ajili ya maendeleo ya Shule ya Sekondari ya Goba iliyopo Kata ya Goba Wilaya ya Ubungo yafanyika mapema Leo tarehe 31 July,2021 lengo likiwa ni uchangiaji wa ujenzi wa uzio wa shule hiyo ambayo inatarajia kuanzisha Elimu ya kidato Cha tano na sita
Akiongea wakati wa hafla hiyo mdau wa maendeleo ndg. Watson Mwakalila aliwataka walimu na wanafunzi kuhakikisha Wana tunza Mali za shule iliziweze kudumu
Aidha Watson ametoa matofali 4,000 kwaajili ya kuanzia msingi wa uzio wa shule hiyo ambayo tayari ujenzi wa bweni kwa wanafunzi wa kidato Cha tano na sita umekamilika
Aidha aliendesha zoezi la ukataji wa keki ambalo alitoa kiasi Cha shilingi laki mbili na kuendesha zoezi la fund rising kiasi Cha shilingi 433,350 cash ilipatikana, 780,000 ilikua ni ahadi, loli mbili za mchanga, tofali 700 na mifuko 10 ya cement kwaajili ya kuendeleza ujenzi wa uzio huo na kuwapa zawadi walimu wanaofanya vizuri katika ufundishaji pamoja na wanafunzi waongoza katika masomo yao
Aliendelea kutoa ahadi ya kuhakikisha anawashirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo ili waweze kusaidia maendeleo ya shule
Nae Mwakilishi wa Mkurugenzi mbaye pia ni Afisa Elimu sekondari Manispaa ya Ubungo Hilda Sharanda amemshukuru Ndg.Watson kwa mchango wake katika kuleta maendeleo kwa wana Goba na kuto salam za shukrani kutoka kwa Mkurugenzi wa Manispaa y Ubungo kwa wana Goba
Alikadhalika Makamu Mkuu wa shule hiyo Pilly Ramadhani ameshukuru kwa zoezi hilo kwenda salama na kusoma taarifa ya toka kuanzishwa kwa shule hiyo ambayo inaendelea kukua na kupata maendeleo
Sambamba na hayo Bi.marry isac mmoja wa wazazi wa wanafunzi wanaosoma Goba sekondari ameushukuru uongozi wa shule pamoja Ndg.Watson kwa harambee hiyo ya uchangiaji wa uzio wa shule na kuhaidi kushirikiana na uongozi wa shule kuleta maendeleo ya Shule na kuhakikisha wanafunzi wanakuwa katika mazingira bora
NB.Goba day ni hafla iliyofanyika kwa ushirikiano Kati ya walimu na wazazi kwa lengo la kutatua changamoto za shule na uchangiaji wa uzio wa shule hiyo
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa