- Mwakilishi wa Shirika la Caritas International, Germany Anna Patzke Salgado amefika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri James ili kujadili mambo mbalimbali yanayohusu biashara haramu ya usafirishaji binadamu.
- DC Kheri ameeleza kuwa biashara hiyo kwa ipande wa Tanzania na maeneo mengine duniani ipo kutokana na hali ya umasikini na uelewa mdogo wa wananchi juu ya biashara hiyo
- Aidha biashara hiyo imezidi kupungua kwa kiasi kikubwa hasa katika maeneo ya mjini na serikali inaendelea kupinga vikali biashara hiyo haramu
- Kwa upande wake mwakilishi wa shirika hilo, Anna Salgado ameshukuru kwa ushirikiano aliopatiwa na ofisi ya Wilaya ya Ubungo na wao kama shirika la Caritas International, Germany wapo tayari kushirikiana kukomesha biashara hiyo kwa wilaya ya Ubungo na Tanzania kwa ujumla
- Ndugu Anna Salgado ameambatana na Maofisa wa shirika la DMI ambapo ni wadau wakubwa kwa wilaya ya Ubungo kwenye kukabiliana na biashara hiyo haramu.
@caritas_international
#ubungoyetufahariyetu
#ubungoyakibingwa
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa