Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri James amewatoa hofu wananchi na watumiaji wa Stendi kuu ya Mabasi ya Magufuli iliyopo Mbezi kuwa Hakuna mgomo wowote wa mabasi katika Kituo hicho na huduma zinaendelea kutolewa kama kawaida ikiwemo usafirishaji wa abiria.
Kheri, ametoa kauli hiyo leo tarehe 25 julai,2022 asubuhi alipotembelea kituoni hapo kwa lengo la kuangalia utoaji wa huduma za usafiri na usafirishaji katika kituoni hapo na kueleza kuwa hakuna mgomo wa madereva wa mabasi kwenye kituo hicho, hivyo watu waendelee na shughuli zao kama kawaida
Aidha, Kheri amewashukuru watoa huduma kwa ushirikiano mkubwa wanaoutoa kwa Halmashauri kwani kituo hicho kimetulia na kazi zinaendelea vizuri, hivyo ondoeni hofu kabisa kwani hali ni shwari na hakuna linalokwamisha shughuli zozote zisiendelee katika kituo.
“Niwakumbushe jambo moja, kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya ubungo inajukumu la kulinda na kuleta Amani na kwa kuzingatia hilo nijukumu letu kutoa ushirikiano kwa wannchi wetu na tuko tayari mda wote ili mradi mfate utaratibu” alisistiza Kheri.
Kheri ametumia nafasi hiyo kuwaeleza wananchi na watumiaji wote wa kituo kuwasilisha changamoto kwa uongozi ili zitatuliwe na kutumia njia ya majadiliano kutatua changamoto zinazojitokeza na Serikali ipo tayari kutoa ushirikiano “muachane na migomo au kuhatarisha usalama wa kituo”
“Ulinzi na usalama wa kituo chetu ni muhimu sana yule atakayechochea uvunjifu wa amani na serikali haitasita kuchukua hatua" amesisitiza Mhe. Kheri.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa