Mapema leo Januari 9, 2023 mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri James pamoja na wataalamu kutoka idara ya elimu msingi na Sekondari wa Manispaa ya Ubungo wamefanya ziara ya kuona mapokezi ya wanafunzi wapya wa darasa la awali, darasa la kwanza na kidato cha kwanza katika shule mbalimbali za Manispaa ya Ubungo
Ziara hiyo imekuja leo kufuatia kufunguliwa kwa shule za msingi na sekondari za umma na binafsi kote nchini kwa mwaka mpya wa masomo 2023 ambapo Mkuu wa Wilaya ametembelea shule ya sekondari Mburahati, shule ya msingi Amani, shule ya sekondari Manzese pamoja na shule ya msingi Kimara.
Lengo la Ziara hiyo ni kuona mapokezi ya wanafunzi hao katika shule zao pamoja na kuongea na wanafunzi pamoja na wazazi waliowapeleka watoto wao kuhusu dhamira ya dhati ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha elimu bure inawafikia watoto wote bila kuwa na changamoto yoyote
"Tunamshukuru Mhe. Rais kwa kuleta elimu bure kwa shule za msingi na sekondari kote nchini. Na kwa sisi Ubungo tunahakikisha hakuna mwanafunzi yoyote atakayerudishwa nyumbani kutokana na sababu yoyote ile" Alisema
Aidha kwa upande mwingine Mhe.James amesema wazazi wasihusishwe kwenye michango yoyote ya shule na kama kuna ulazima wa mchango wowote katika shule yao utahitajika basi ni sharti utaratibu ufatwe ili kibali kitolewe na yeye mwenyewe Mkuu wa Wilaya na si vinginevyo
Nae Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndugu Beatrice Dominic amesema shule zote za Manispaa ya Ubungo zimewapokea vizuri wanafunzi wake na zoezi la uandikishaji linaendelea ambapo mpaka hivi sasa wanafunzi walioandikishwa kwa shule za serikali kwa darasa la awali ni 2,010 sawa na asilimia 37, darasa la kwanza ni 11,331 sawa na asilimia 83 na kidato cha kwanza ni 15,800 ambayo ni zaidi ya asilimia 50.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa