Leo tarehe 08/11/2022 Wageni kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakiwemo waheshimiwa madiwani na wataalamu wa Halmashauri hiyo wamefanya ziara ya kutembelea Manispaa ya Ubungo lengo ikiwa lengo ni kujifunza na kubadilishana juu ya ukusanyaji wa mapato na uendeshaji wa Kituo cha Mabasi cha Magufuli “Magufuli Bus Terminal”.
Akiongea Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Manispaa ya Ubungo Dkt Peter Nsanya amewaeleza wageni hao namna Manispaa hiyo inasimamia ukusanyaji wa mapato kwa ufanisi ambapo kila kata inamlezi wake ambao ni wakuu wa idara na Vitengo na maafisa biashara ambao wamekuwa wakishirikiana na viongozi wa Kata wanazozilea katika kuhakikisha mapato yanakusanywa kwa usahihi na ufanisi
Nsanya ameendelea kueleza kuwa uwepo wa Kituo cha Magufuli umekuwa ni chachu ya kuongeza mapato kwa Manispaa hiyo ambapo kwa mwaka kituo hicho kinakusanya shilingi Bilioni 5 kutoka kwenye vyanzo vyake ikiwemo ushuru wa kuingilia kituoni, vyooni, bajaji na pikipiki, hoteli inayosimamiwa na mzabuni, parking za kulaza magari, Ada ya kuingiza na kutoa mabasi kituoni na upangishaji wa fremu za biashara.
Sambamba na maelezo hayo wageni hao wamefanikiwa kujua namna kituo hicho kinaendeshwa na kusimamiwa kwa ufanisi kwa maslahi ya wanaubungo.
Nae Mhe. Kheri James Mkuu wa Wilaya ya Ubungo amesema Mkoa wa Dar es Salaam ambao Wilaya ya Ubungo ipo ndani yake na Mkoa wa Mwanza inakimbizana katika wingi wa watu hivyo ni lazima kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake na hivyo ni vyema kubadilishana uzoefu kwa mazuri yanayofanywa na Halmashauri za mikoa hiyo.
James ameendelea kueleza Stendi kubwa ya Mkoa wa Dar es salaam ipo Ubungo hivyo ni vyema wageni hao kujifunza namna kituo hicho kinaendeshwa ili kupata uzoefu wa kwenda kuendesha kituo chao cha Nyegezi na amewapongeza kwa ujenzi wa Kituo hicho cha kisasa.
Kwa upande wake Kaimu Naibu Meya wa Jiji la Mwanza Mhe. Hamidu Selemani Said ametoa shukrani kwa mapokezi mazuri waliyoyapata pamoja na fursa ya kujifunza mambo mengi mazuri yanayofanywa na Manispaa ya Ubungo
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa