Wataalam kutoka Halmashauri ya Jiji la Tanga, Leo tarehe 14.3.2021 wamefanya ziara ya kikazi katika Manispaa ya Ubungo Lengo ikiwa ni kujifunza namna ya uendeshaji na usimamizi wa Kituo Cha Mabasi Cha Magufuli kilichopo Mbezi ikiwa ni maandalizi ya kufungua Kituo Chao kipya kilichopo Kange Jijini humo
Kiongozi wa msafara huo Mchumi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Bi. Mariam Chihimba amesema kuwa Lengo la ujio wao ni kuona namna Kituo kinavyoendeshwa kwa kuzingatia namna bora ya upandishaji na uendeshaji wa Kituo hicho na pia swala zima la ukusanyaji wa mapato ili kuweza kupata elimu ambayo itaenda kuwasaidia katika uendeshaji wa stendi yao mpya
"Tumefurashishwa na mfumo wa pangisha ambao Ubungo waliweza kuutumia" na yote tuliyojifunza ikiwemo matumizi ya Tehama ikiwemo Pos machine, ufungaji wa camera(CCTV) Kama ulinzi wa Kituo na pia swala zima la usimamizi wa Kituo ambao Meneja wa Kituo ameweza kutuelezea" alieleza Mariam
Mariama pia ameishukuru Manispaa ya Ubungo kwa ukarimu walioupata na kuweza kujifunza mengi kuhusiana na Kituo hicho pia swala zima la ushirikiano uliopo Kati ya watalaam wa menejimenti ya Manispaa ya Ubungo ulivyo kwani umekuwa ni mfano tosha wakuigwa
Aidha Afisa utumishi Manispaa ya Ubungo Selemani kateti ameishukuru Halmashauri jiji la tanga kwa kuichagua Manispaa ya Ubungo kuwa ya mfano kuwapa elimu na pia ameendelea kusisitiza kuhusu swala la mahusiano kuendelea kudumishwa na kuwakaribisha tena Manispaa ya Ubungo
"Aliendelea kwa kusema kuwa anashukuru kwa waliyojifunza na kuwaeleza kuwa Kituo kinaendelea na Ujenzi kwaiyo hata nyinyi mnaweza mkaendelea na utoaji wa huduma huku Kituo kikiendelea kujengwa"
N.b Mradi wa Ujenzi wa Kituo ulianza Mwaka 2019-2020 na kujengwa kwa miezi 18, Kituo kinauwezo wa kupaki mabasi 108 na pia kina majengo mbalimbali ikiwemo utawala, sehemu ya kushusha na kupakia abiria,sehemu ya abiria n.k
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa