Manispaa ya Ubungo imefanya Baraza Maalum la kujadili taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali katika ukumbi wa Little Flower uliopo Mbezi.
Baraza hilo limeongozwa na Kaimu Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo Mhe.Ramadhani Kwangaya, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic ambaye ni Katibu wa Baraza.
Baraza hilo limehudhuriwa na Mkaguzi Mkuu wa Nje-Ubungo Ndg. Suleiman Mwaliwale, Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Serikali za Mitaa Marry P. Assey,Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg. James Mkumbo, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya,Maafisa Tarafa wa Wilaya ya Ubungo, Madiwani na wataalam kutoka Manispaa.
Baraza hilo maalum lilikuwa na lengo la kupitia hoja za Mkaguzi wa nje na wajumbe wa Baraza kuzijadili kwa ajili ya kuzitolea majibu kabla hazijaenda kwenye Kamati ya Bunge.
Baraza lilikubaliana na hoja ambazo zilitolewa na mkaguzi wa hesabu za Serikali na kuitaka Halmashauri izingatie maoni ya kamati ya fedha yaliyotolewa kwa mwaka wa fedha 2019/2020 na kufanyiwa kazi.
Vilevile Baraza lilipendekeza udhibiti uongezeke katika suala la mapato.
Pia Baraza lilishauri mkandarasi anaehusika na ujenzi wa jengo la Halmashauri kumaliza kazi kwa wakati.
Aidha Ndg. Suleiman Mwaliwale alitoa pongezi kwa Menejimenti ya Halmashauri na Madiwani kwa juhudi zilizofanyika kupata hati safi kwa miaka mitatu mfululizo.
Nae Mary Assey aliipongeza Manispaa ya Ubungo na Menejimenti kwa kupata hati safi kwa miaka mitatu mfululizo tangu kuanzishwa na kwa kujibu hoja ipasavyo na kuzifunga baadhi kama zilivyotolewa na Mkaguzi wa nje.
"Niwaombe mhakikishe kuna ukusanyaji mzuri wa mapato na kukusanya madeni na kuyafuatilia, bajeti isimamiwe na manunuzi na matumizi ya fedha yafuate taratibu." Aliongezea Marry Assey.
Katibu Tawala wa Wilaya alisisitiza hela inayokusanywa ihakikishwe inapelekwa benki. Vile vile watumishi wafanye kazi kwa kufuata taratibu na sheria.Watendaji ambao wana madeni ya muda mrefu wachukuliwe hatua.
Mwisho Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic aliwashukuru kwa juhudi na ushirikiano unaoendelea kutolewa na Ofisi ya Ras pamoja na waheshimiwa madiwani na kuahidi kufanyia kazi ushauri uliotolewa.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa