Kikao hicho kimefanyika leo katika ukumbi wa LAPAZ uliopo luguruni na kufunguliwa na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ubungo Dr. Peter Nsanya
Kikao hicho kimehudhuriwa na watumishi wa Idara ya Afya, Wenyekiti wa Kamati ya vituo vya afya na Mwenyekiti wa bodi ya Afya Manispaa ya Ubungo. Dhumuni la kufanya kikao hicho cha tathmini ni kuona maendeleo na changamoto ambazo idara imezipata kwa mda wa miezi sita kuanzia julai hadi desemba.
Wakati akifungua alipongeza watumishi wote kwa juhudi ambazo wamezifanya kwa nusu mwaka 2019/2020 na wenyeviti ambao wanasimamia katika vituo vya Afya na kukumbushana kuhusu majukumu yanayofanyika na kusimama imara katika kuleta maendeleo katika vituo vya afya, wenyeviti kuhakikisha wanaunganisha ipasavyo wananchi na manispaa kwa kuhakikisha wanasikiliza changamoto zao na kuzitatua, na kudumisha mahusiano baina ya manispaa na wananchi wa Wilaya ya Ubungo. Si hayo tuu lakini pia kuhakikisha wanaitunza miundombinu ya vituo vya Afya.
Alimaliza kwa kufunga kwa kuwashukuru wageni wote na kusisitiza juu ya ufanyaji kazi bora katika vituo vyao vya afya na zahanati.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa