Mkuu wa Idara ya Utawala na Utumishi Manispaa ya Ubungo Selemani Kateti amefanya kikao na watumishi walio chini ya Idara ya Utawala na Utumishi na kuwakumbusha utekelezaji wa majukumu yao wanapokuwa katika Ofisi zao kwa kusimamia majukumu yao na kufata kanuni, taratibu na Sheria za kazi
Kikao hicho kimefanyika Leo Agosti 10, 2022 ambapo Watumishi hao walipata nafasi ya kushiriki kutoa Mapendekezo na maoni mbalimbali ili kuimarisha utendaji kazi
Kateti, aliwataka watumishi hao Kila mmoja kujua nafasi yake anapokuwa katika kituo Chake Cha kazi ili kuboresha utendaji kazi na utoaji wa huduma .
"Tujifunze kujiamini na mkasimamie ipasavyo watu mnao waongoza katika Vituo vyenu vya kazi" aliongeza Kateti.
Aliendelea kwa kusisitiza Kila mmoja kushiriki katika maswala ya kijamii ili kupeana nguvu na faraja mtu anapopata changamoto na hata matukio ya furaha.
Aidha, Kateti alisema pia ushirikiano ni muhimu, upendo, kufata maadili ya kazi, kanuni, Sheria na taratibu za kazi ni Jambo la msingi Kwakila mmoja wetu kulizingatia.
Katika swala la ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri watendaji waliomba ushirikishwaji wa maafisa biashara ili kufanya kazi kwa pamoja na kuomba uwepo wa kikao cha tathmini ambacho kitalenga kuboresha na kuongeza mapato ya Halmashauri.
Aidha, watumishi hao walimpongeza mkuu wa idara hiyo kwa kusimamia vyema changamoto wanazozipata na kuahidi kuendelea kufanya kazi kwa uweledi.
|
|
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa