Mbunge wa Jimbo la Kibamba Manispaa ya Ubungo kwa kushirikiana na Uhuru FM Leo tarehe 30 Julai, 2022 wamefanya mazoezi ya matembezi ya haraka (Jogging) yaliyoanzia eneo la Kibanda cha Mkaa hadi Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo lililojumuisha vikundi mbalimbali vya Jogging Lengo ikiwa ni kuhamasisha zoezi la Kitaifa la Sensa ya watu na makazi 23 Agosti, 2022.
Sambamba na zoezi hilo kulikuwa na michezo mbalimbali ikiwemo kukimbia na mayai mdomoni, kucheza bao na mengineyo ambapo zawadi mbalimbali ziligaiwa kwa washindi wa michezo hiyo.
Akiongea Mhe. Issa Mtemvu Mbunge wa Jimbo la Kibamba ametoa wito kwa wananchi wa Manispaa ya Ubungo hususani Jimbo la Kibamba kujitokeza kuhesabiwa na kutoa taarifa sahihi ili kuiwezesha Serikali katika kupanga mipango yake kwa usahihi.
Mtemvu ameendelea kueleza kuwa kila mtu akihesabiwa takwimu hizo zitasaidia Serikali katika kupanga mipango ya sekta ya afya, kuboresha miundombinu na kadhalika.
Aidha, Mtemvu amewapongeza viongozi mbalimbali wa dini wakiwemo Masheikh, Wachungaji, Mapadri na Maaskofu kwa kuendelea kuhamasisha zoezi hili muhimu kama ambavyo Serikali imekuwa ikifanya na ametoa shukrani kwa wananchi na vikundi mbalimbali vilivyojitokeza kushiriki zoezi hilo.
Nae Ndg. Pius Ntiga Mhariri wa Habari Uhuru FM ameeleza kuwa matembezi hayo ni maandalizi ya kampeni yao ya Sensa Marathoni Uhuru FM yanayotarajia kuanza mwezi ujao ikiwa ni pamoja na Kuisaidia Serikali katika kuhamasisha zoezi la Sensa ya watu na makazi kwa wananchi.
Kwa upande wake Mhe Hassan Silaji Mwasha Naibu Meya wa Manispaa ya Ubungo ametoa pongezi kwa wananchi na vikundi mbalimbali vilivyoshiriki matembezi hayo ya kilomita 5 na ameeleza kuwa wananchi wa Jimbo la Kibamba wapo tayari kuhesabiwa ili kuiwezesha Serikali kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa