Kamati ya Mpya ya Fedha na Uongozi Manispaa ya Ubungo imetembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Shule Maalum ya wasichana ya Mkoa inayojengwa katika Kata ya Kwembe ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya kamati hiyo.
Baada ya kujionea utekelezaji wa mradi huo wajumbe wa Kamati hiyo wameridhika na ubora wa mradi huo na kusisitiza mradi kukamilika kwa wakati ili shule hiyo ianze kuchukua wanafunzi.
Aidha, Wajumbe wamepongeza hatua iliyofikiwa ya utekelezaji wa mradi huo ambapo mpaka sasa mradi umefika 45%
Kwa upande wake Mkandarasi anayejenga mradi huo ameihakikishia kamati hiyo kuwa mradi huo utakamilika kwa wakati kama mkataba unavyoelekeza.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa