Kamati ya afya Msingi ngazi ya Wilaya yafanya kikao kazi kuhusiana na maswala ya uhamasishaji wa chanjo ya UVIK0- 19
Akifungua kikao hicho tarehe 17,septemba,2021 Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe.Kheri James ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati hiyo ameendelea kuwakumbusha wananchi kuhakikisha wanaendelea kuchua tahadhari Kama zinavyotolewa na wizara ya afya na kupata chanjo ya UVIKO -19 ambayo inatolewa bila malipo nchini kote
Aliendelea kusema kuwa Chanjo ya UVIKO-19 ni hiari Ila tunaendelea kuhamasisha wananchi kupata chanjo hiyo kama kinga
Aidha ameendelea kusisitiza kwa wajumbe kuhakikisha usimamizi na kuratibu shughuli kazi ya utoaji wa chanjo inafanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kuwafikia walengwa wote ambao wapo katika wilaya
Akisoma taarifa fupi kuhusiana na utoaji wa chanjo ulipofikia mpaka sasa Mratibu wa chanjo Manispaa ya Ubungo Ndg.Boniphasi Katikilo amesema kuwa mpaka sasa watu 14,921 wamefikiwa Toka chanjo ilipotolewa ambapo wanawake ni 5,640 sawa na 36% na wanaume ni 9,281 sawa na 64%
Aliendelea kusema kuwa shughuli za utekeleza wa utoaji wa elimu unaendelea na kuhamasisha jamii na taasisi mbalimbali kuhakikisha wanaweka vifaa vya kutakasa mikono katika maeneo yao
Pia kusimamia mwongozo ambao unawataka wananchi kuendelea kufanya shughuli zao za kiuchumi na jamii sambamba na kubadili tabia zao huku wakizingatia mbinu za kujikinga na ugonjwa huo
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa