Kamati ya Fedha na Utawala Manispaa ya Ubungo imetembelea mabanda waliohamishiwa wajasiriamali wadogo waliokuwa wanafanya biashara kituoni hapo katika maeneo yasiyo rasmi, ikiwemo wale waliokuwa kwenye eneo la kupakia na kushusha abiria hali ambayo ilikuwa inaharibu mwonekano wa kituo pamoja na kusababisha usumbufu kwa abiria.
ziara hiyo imefanyika Oktoba 18,2021 ikiwa ni utekelezaji wa majukumu ya Kamati hiyo kila baada ya miezi mitatu.
Kamati iliamua kutembelea eneo hilo ili kuona utekelezaji wa agizo la Serikali la kuhakikisha wamachinga waliokuwa wanafanya Biashara Katika maeneo ambayo siyo rasmi wamehamia kwenye maeneo yaliyotengwa.
Wajumbe wa Kamati hiyo wakiongozwa na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mhe. Jaffary Juma Nyaigesha amewapongeza wajasiriamali hao kwa kuhamia Katika eneo la muda lililopangwa ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Serikali.
Pamoja na pongezi hizo, Nyaigesha amewataka wajasiriamali hao kuzingatia usafi wa mazingira kwa ajili ya afya zao na kutunza mazingira ya kituo
Akitoa maelezo mbele ya kamati hiyo, Afisa Biashara wa kituo hicho Geofrey Mbwana amesema kuwa jumla ya wajasiriamali 447 walihamishiwa kwenye mabanda hayo ambapo Kati ya hao wajasiriamali 236 walikuwa kwenye eneo la kupakia na kushusha abiria
"Kwa sasa tatizo la wajasiriamali waliokuwa maeneo yasiyo rasmi katika kituo limeisha baada ya kukubali kuhamia kwenye mabanda ya muda yaliyojengwa na Manispaa kwenye kituo hicho ili wayatumie kwa muda wakati jengo rasmi la baba na mamalishe halijajengwa"
Aidha, wajumbe wa Kamati hiyo walitembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Kituo cha mabasi cha Magufuli, Hospitali ya Wilaya iliyopo Kimara Baruti, Ujenzi wa madarasa matatu shule ya Msingi msewe na shule ya Msingi Matosa
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa