Kamati ya Fedha na Uongozi Manispaa ya ubungo pamoja na wataalamu wakiongozwa na Mstahiki Meya Mhe. Jaffary Juma Nyaigesha imefanya ziara ya mafunzo katika Halmashauri ya jiji la dodoma, lengo ikiwa ni kupata uzoefu wa ujenzi wa mabanda ya wamachinga kutokana na jiji hilo kufanya vizuri katika kutekeleza mradi huo.
Ziara hiyo ni utekelezaji wa agizo la Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Innocent Bashungwa alipotembelea Kituo cha Mabasi cha Magufuli mwishoni mwa mwezi Mei ambapo moja ya kero iliyojitokeza ni mazingira ya wamachinga kutoendana na mahitaji yao.
Akizungumza baada ya kutembelea mradi wa ujenzi wa mabanda ya kisasa ya machinga jijini humo, mstahiki Meya wa Manispaa ya ubungo ameeleza kuwa ziara hiyo imewapa mwanga mzuri wa namna ya kwenda kutekeleza mradi wa ujenzi wa mabanda ya wamachinga kwa ubora na usasa zaidi.
Pamoja na mradi wa ujenzi wa mabanda ya machinga, jiji la dodoma pia linatekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo masoko, Hoteli, ukumbi na maeneo ya kupumuzikia ambayo ni miradi ya uwekezaji na inayoliingizia jiji mapato ya ndani kwa uhakika.
Baadhi ya miradi iliyokamilika ikiwemo soko, stendi na maeneo ya wazi tayari jiji linakusanya fedha kutoka kwenye Miradi huku miradi ya ujenzi wa hoteli mbili za kisasa ukiwa hatua nzuri za ukamilishaji.
Mradi wa ujenzi wa Soko la machinga
Akiieleza kamati ya fedha ya Ubungo siri ya mafanikio hayo Mstahiki meya wa Jiji la Dodoma Dkt Mwamfupe alisema kuwa udhubutu wa maamuzi, ushirikiano na ushirikishaji wadau ndio vimepelekea mafanikio hayo ya kuweza kuwa na miradi mikubwa ya uwekezaji ikiwa ni suluhisho la kuwa na vya uhakika wa mapato na kupelekea kutoa huduma bora kwa wananchi.
Dkt Mwamfupe anasema "Haya mafanikio sio fedha ni udhubutu wa kuamua kufanya jambo linaloweza kuwezesha jiji kutoa huduma kwa kutumia fedha za mapato ya ndani bila kutegemea fedha za Serikali Kuu lakini pia ni vyanzo vya uhakika"
Mradi wa ujenzi wa Ukumbi wa kisasa eneo la Mtumba
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa