- Leo Novemba 9, 2022 kamati ya huduma za Uchumi, Afya na Elimu imefanya ziara katika mradi wa shule maalumu ya sekondari ya wasichana inayojengwa katika eneo la Njeteni kata ya Kwembe pamoja na kutembelea hospital ya Palestina iliyopo kata ya Sinza.
- Kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake ambaye ni diwani wa Viti Maalumu Mhe. Liberata Samson ilipotembelea miradi hiyo imegundua madhaifu mbalimbali ambapo wamewaelekeza wakandarasi kufanyia kazi mapema kutoka sasa ili kukabidhi miradi ambayo itakua imekidhi vigezo vyote na inayoonesha thamani ya fedha ambayo serikali imeweka
- Katika Mradi wa shule hiyo ya wasichana ambao unajengwa na mkandarasi Bandiko Construction limited ambapo mradi huo una thamani ya shilingi Bilioni 3 na kwasasa umefika zaidi ya asilimia 90 ukitarajiwa kukamilika Disemba 30. Mradi huo una jumla ya madarasa 12, maabara 4 pamoja na mabweni 3
- Katika ziara hiyo Kamati imebaini baadhi ya mapungufu katika mradi huo ikiwemo kutokuridhishwa na uimara wa frame za milango hivyo wamemuagiza mkandarasi kubadili frame hizo mara moja
- Kwa upande wa hospitali ya Palestina iliyopo Sinza, kamati imekagua mradi wa umaliziaji ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje OPD lenye thamani ya shilingi milioni 326. Akizungumza wakati wa kuwasilisha ripoti ya mradi huo kaimu mganga mfawidhi wa Hospitali hiyo Dkt. Elizabeth Ngulo amesema kuwa mradi huo ambao umefikia asilimia 93 ulitarajiwa kukamilika Oktoba 30 lakini changamoto kadhaa zimekwamisha mradi huo kukamilika kwa wakati ikiwemo changamoto ya kuchelewa kwa malipo kwa mafundi hali inayopelekea nguvu kazi kupungua
- Kamati imebaini mapungufu mbalimbali katika mradi huo ikiwemo ubora wa madirisha yaliyowekwa na hivo wamemuagiza mkandarasi kurekebisha haraka kutoka sasa kabla ya kukabidhi mradi
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa