Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic leo septemba 7, 2021 amepokea ripoti ya Kamati maalumu iliyoundwa kutembelea na kuchunguza maeneo ya wazi katika kata tano za Manispaa hiyo ikiwa ni moja ya chanzo cha Mapato kwa Manispaa
Kamati hiyo ilitembelea na kukagua maeneo yaliyopo katika kata za Sinza, Manzese, Mburahati, Goba na Makurumla.
Akiongea wakati wa kukabidhi ripoti, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Eliamu Manumbu amesema kuwa, Kamati imefanikiwa umetembelea maeneo 285 ambapo maeneo 51 ni ya wazi, 211 vizimba vya maji na maeneo mapya 23 yanayoweza kukusanya kiasi cha shilingi 564,352,960 kwa mwaka mzima kwa kata tano zilizotembelewa na kukaguliwa.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, Beatrice Dominic {wa kwanza kulia} akikata utepe wa baadhi ya ripoti za uchunguzi wa maeneo ya wazi katika kata tano ikishuhudiwa na mwenyekiti wa kamati hiyo Eliamu Manumbu {katikati}
Aidha, Mwenyekiti ameendelea kueleza kuwa, Kamati imependekeza zoezi hilo lifanyike kwenye kata 9 zilizobaki ili kubaini maeneo hayo ambayo ni chanzo mikubwa cha Mapato kwa Manispaa hususani katika kipindi hiki ambacho bajeti ya Manispaa hiyo imepanda kutoka bilioni 18 Hadi kufikia bilioni 27 Kwa mwaka huu wa fedha.
Mwenyekiti wa Kamati amefafanua kuwa milioni 564.4 zilibainishwa na Kamati kukusanywa katika maeneo hayo haijajumuisha tozo za maeneo ya wazi ambayo ukubwa halisi haukupimwa wakati Kamati ikifanya uchunguzi, kutokana na sababu hiyo Manispaa inauwezo wa kukusanya mapato mengi zaidi ya hayo yaliyobainishwa.
Kamati hii iliyojumuisha waheshimiwa Madiwani, wataalamu, na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ni utekelezaji wa azimio la mkitano wa Baraza la Madiwani lililoketi mwezi April mwaka huu lengo ikiwa ni kuyatambua maeneo hayo ikiwa ni moja ya chanzo cha Mapato ya Halmashauri.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa