Kamati ya Kudhibiti Ukimwi Manispaa ya Ubungo leo tarehe 18, Mei 2022 wametembelea Mtaa wa Muungano Kata ya Manzese kwa ajili kujionea maeneo hatarishi (madanguro) ikiwa ni pamoja na kugawa kinga kwa makundi hatarishi.
lengo la kamati kutembelea maeneo hayo hatarishi ni kuendeleza mapambano dhidi ya UKIMWI na kuendelea kuwapa elimu ya kujikinga na ugonjwa huo hatari ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu ya madhara ya kazi hiyo haramu wanayoifanya.
Akiongea katibu wa kamati hiyo Mercy Ndekeno amewaeleza wadada hao wanaotumia miili yao ili kujingizia kipato watumie fursa mbalimbali za kujikwamua na umaskini na kuacha kazi haramu.
Alikadhalika, mwenyekiti wa kamati hiyo amewaomba viongozi wa dini kuendelea kutoa elimu ya dini kwa makundi hatarishi.
Aidha asasi za kiraia kuendelea kushirikiana vyema na serikali ili kuendeleza mapambano dhidi ya ukimwi ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati imara yakuwafanya mabinti na wadada wanaojiuza kuacha kazi hiyo kwa kuwawekea misingi bora ya kuwasaidia kujikwamua kiuchumi na kuwaaminisha wanaweza kuendelea kuishi kwa kufanya shughuli halali za kijamii na sio ya kuuza miili yao.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa