Kamati ya kudhibiti UKIMWI Manispaa ya Ubungo leo 14 january,2022 imetembelea Baraza la watu wanaoishi na VVU la Wilaya(Konga) lililopo Kata ya Msigani na kujionea shughuli zinazosimamiwa na baraza hilo
Aidha Miongoni mwa baraza hilo Kuna Vikundi wezeshi vya Watu wanaoishi na VVU katika Kata zote 14.
Na pia Kamati ilifanikiwa kukutana na kikundi Wezeshi Cha Saranga VICOBA na kujionea shughuli zinazofanyika kwenye kikundi ikiwemo utengenezaji wa sabuni, mafuta , pafyumu , batiki na usimamizi wa majukumu yao Kama kikundi.
Akiwasilisha taarifa ya Konga Katibu Neema Duma alisema kuwa wamefanikiwa Kutoa ELIMU kwa Jamii, wamefanikiwa kubaini Maeneo hatarishi yanayoweza kusababisha ongezeko la maambukizi ya VVU na kusambaza kondom katika Maeneo tofauti n.k
Sambamba na hayo Wana Konga waliwasilisha maombi kwa kamati iweze kuwaisadia kupata ofisi ya kudumu kwaajili ya shughuli zao za Kila siku
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa