- Leo Septemba 28, 2022 Kamati ya kudumu ya Bunge - Viwanda, Biashara na Mazingira chini ya Mwenyekiti wake Mhe. David Kihenzile imetembelea eneo la viwanda ambalo lipo chini ya taasisi ya Export Processing Zones Authority (EPZA) Katika eneo la Ubungo External Jijini Dar es Salaam kwaajili ya kukagua mpango wa kutunza mazingira kiwandani hapo
- Kamati imeridhishwa na mfumo mzima wa utunzaji wa mazingira ikiwemo namna ambavyo maji yanayotumika kiwandani hapo yanavyotunzwa na kurudishwa tena kwenye matumizi (Recycling)
- Kamati imeshauri viwanda vingine kuiga mfumo huo ili kuhakikisha mazingira yanalindwa kwa manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla
- Katika upande Mwingine Kamati imeshauri umuhimu wa kutumia taka zinazozalishwa kwenye viwanda mbalimbali zitengeneze mbolea ili kuhakikisha tunakua na uchumi wa viwanda ambao unatumia fursa zote
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa