Kamati ya Lishe Wilaya ya Ubungo imefanya kikao katika ukumbi uliopo Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa lengo la kujadili utekelezaji wa Afua za Lishe.
Kikao hicho kimeongozwa na Katibu Tawala Wilaya ya Ubungo Ndg. James Mkumbo na Bi.Neema Mpanduji mwakilishi wa Mganga Mkuu ambaye pia ni Mratibu wa Ukimwi, Afya pamoja na Wakuu wa Idara ambao ni wajumbe.Katika kikao hicho wajumbe walipata nafasi ya kuwasilisha taarifa zao juu ya namna walivyotekeleza mkataba wa Lishe.
Wakati akifunga kikao hicho Katibu Tawala aliwapongeza wajumbe kwa jitihada wanazozifanya kutekeleza mkataba wa Afua za Lishe.
Aidha Katibu Tawala alimwelekeza Mkurugenzi ahakikishe fedha yote ambayo ilitengwa kwenye bajeti kuhusu masuala ya lishe inatolewa na itumike kama maelezo ya mkataba wa afua za lishe unavyoelekeza
”Lishe ni kama moyo wa mwanadamu na tukikosea hapo athari zake zinakuwa za kudumu” alisema Katibu Tawala.
Alisisitiza kuwa mkataba wa Afua za lishe lazima usimamiwe madhubuti na likisimamiwa vizuri baadhi ya hela ambazo zinatakiwa kwenda kwenye Afya zitatumika kwenye miradi mingine. Vile vile Kamati ihakikishe kwamba hela yote iliyopangwa inatumika ipasavyo kwani tunaelekea kumaliza mwaka wa fedha.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa