Tarehe 7 mei 2021 kamati ya michezo Wilaya ya Ubungo na Uongozi wa cha mpira wa miguu Ubungo (UFA) wamefanya kikao kujadili utendaji kazi wa chama cha mpira wa miguu (UFA) Ubungo na maswala mbalimbali ya kukuza michezo katika Wilaya ya Ubungo
Kikao hicho kimehudhuliwa na mwakilishi wa Katibu Mkuu Baraza la michezo Taifa Mirinde Mahona, Afisa michezo wa Mkoa wa dar es salaam Adolf Halii, Wataalam wa Manispaa ya Ubungo na wadau wa michezo wa Wilaya ya Ubungo kutoka chama cha mpira wa miguuu (UFA)
Wakati wa kikao hicho mwakilishi wa Katibu wa Michezo taifa, Mahona aliwashauri wajumbe kuhakikisha wanafata sheria, kanuni na misingi ya utawala bora
Aliendelea kwa kusema kuwa uongozi lazima uhakikishe unatatua migogoro ya chama kwa uweredi ilikuepusha sintofahamu kwa wajumbe katika chama
Nae Afisa michezo Mkoa Ndg Adolf Halii aliwapongeza uongozi wa UFA kwa kufanya kazi zake kwa weredi za kuendesha chama chao na kuwataka kuachana na migogoro ya ndani ya chama ilikikue na kupata maendeleo zaidi
Aliendelea kwa kuwataka UFA kuwa na malengo, uwazi, na kuwataka kuhakikisha wanashirikiana na kamati ya wilaya katika mambo mbalimbali yanayohusu chama chao na klabu
Sambamba na hayo Afisa Utamaduni wa Manispaa ya Ubungo Ritha nguruwe alishauri uongozi wa cha chama mpira wa miguu UFA kuhakikisha umoja na mshikamano katika jumuiya zao za michezo ilikuleta maendeleo katika soka na kuachana na mivurugano na migogoro inayoendelea katika virabu na uongozi
Nae Mjumbe wa kamati hiyo Ndg.Adam bwao alisitiza na kuwaomba wajumbe kutambua Michezo ni ajira na inaangaliwa na watu wengi kwa maendeleo ya watu wa ubungo
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa