Kamati ya Siasa Mkoa wa Dar Es Salaam leo Machi 18, 2022 wamefanya ziara Wilaya ya Ubungo na kupokea taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Wilaya hiyo.
Katika ziara hiyo, kamati imetembelea mradi wa Ujenzi wa madarasa 20 katika shule mpya ya sekondari Makabe ikiwa ni moja ya madarasa 151 yaliyojengwa katika shule 21 kupitia fedha za UVIKO-19 shilingi Bilioni 3.02.
Aidha, Kamati imepongeza Manispaa ya Ubungo kwa juhudi za uendeshaji mzuri wa miradi hiyo kwa kuhakikisha fedha walizopokea zimetekeleza miradi hiyo kwa ufanisi na uweledi
Nae mwenyekiti wa chama Cha Ccm Mkoa Kate Kamba ameagiza miradi yote ya madarasa na madawati kutunza ili iweze kutumika hata kwa vizazi vijavyo
Niwapongeze watalam wa Halmashauri kwa usimamizi mzuri wa mradi, pamoja na Wana Makabe kwa kupata shule ambayo imeenda kutatua changamoto ya kufata shule mbali
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mheshimiwa Kheri James amesema kuwa kufikia Machi, 2022 Wilaya ya Ubungo imepokea kiasi Cha shilingi 18,909,220,309.10 kati ya fedha hizo shilingi 5,817,115,398 ni mapato ya ndani , 12,530,340,827 fedha za ruzuku na shilingi 561,764,083 ni fedha za wadau
Aidha Kheri amewasilisha nyaraka ya Taarifa ya utekelezaji wa miradi kwa Mwenyekiti wa chama Mkoa Mheshimiwa Kate kamba
Aliendelea kwa kusema kuwa kwa upande wa Afya shilingi 3,481,559,956 zimepokelewa kwaajili ya miradi ya maendeleo Kati ya hizo 1,031,000,000 ni mapato ya ndani na shilingi 2,450,559,956 kutoka serikali kuu na wadau
Elimu sekondari imepokea shilingi 9,173,075,421.18 Kati ya fedha hizo shilingi 8,454,891,331 fedha za ruzuku na 677,200,000 fedha za mapato ya ndani
Bilioni 1,714,497,430 zimetolewa kwaajili ya mikopo ya Wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ambapo vikundi 140 vya Wanawake wamepewa 938,707,430, vikundi 69 vya vijana vimepewa 651,240,000 na vikundi 13 vya watu wenye ulemavu shilingi 124,550,000
Elimu msingi 2,238,389,329 kwaajili ya utekelezaji wa miradi ,TASAF imepokea shilingi 167,891,150 kupitia mpango wa kusaidia kaya maskini
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa