Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo tarehe 1/2/2020 imetembelewa na Viongozi wa kamati ya Siasa Mkoa.
Katika ziara hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wa kamati ya Siasa Mkoa Mhe.Kate Kamba Katibu wa Siasa Mkoa Ndg. Zakaria Mwansasu na Viongozi wa kamati ya Chama Wilaya na kupokelewa na wenyeji wao Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe.Kisare Makori na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic.
*Miradi iliyotembelewa ni mradi wa Tanki la usambazaji maji uliopo Kwembe, Mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Ubungo uliopo Kimara, Mradi wa upanuzi barabara ya Morogoro njia nane kuanzia kimara hadi Kibaha, Mradi wa Shule wa ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa na ofisi 1 ya walimu na ukamilishaji wa vyumba 3 vya madarasa shule ya Msingi Mbezi luis, Mradi wa Ujenzi wa fly overs(ubungo interchange), na Mradi wa ujenzi wa barabara ya Korogwe Kilungule.*
Nitoe pongezi kwa jitihada ambazo mmezionyesha katika Miradi tuliyoitembelea, mkaendelee kusimamia vizuri Miradi hiyo ikamilike kwa wakati na tarehe ambazo mmezitaja katika ukamilishaji wa Miradi hiyo ikatimie ipasavyo na kwa wakati. Alisema Mwenyekiti.
Kwa shule hii ya Mbezi luis nimefurahishwa na huendeshaji wa mradi huu na pia jambo ambalo limefanyika la ubunifu katika darasa ambalo linatumika kutolea elimu ya vitendo ikawe mfano na kwa shule nyingine, Nimpongeze pia Mkurugenzi kwa usimamizi na utekelezaji mzuri wa mradi huu wa madarasa na maendeleo ya shule kwa ujumla. Aliongeza Mwenyekiti.
Aidha Mwenyekiti alisisitiza usimamizi wa miradi kwa kuzingatia thamani ya miradi na viwango vya mradi na miradi kusimamiwa kwa umakini, Tunapotembelea miradi tuhakikishe tuna zingatia utekelezaji wa miradi kwa umakini kama viongozi.Pia nipongeze viongozi wa Wilaya ya Ubungo Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi kwa usimamizi na utekelezaji mzuri wa miradi. Aliongeza Mwenyekiti.
Aidha Katibu wa Siasa Mkoa alisisitiza miradi kusimamiwa kwa umakini na kwa kuzingatiwa thamani yake ili kuleta maendeleo.
"Nimesikia changamoto ambayo inaikumba kwa sasa Halmashauri hii kwa kukosa jengo lake la kudumu kitu kinachopelekea wananchi kukosa huduma katika eneo moja na hii imetokana na ofisi kuwa mbalimbali, Mkurugenzi hakikisha mkataba na Mkandarasi ambaye anakwamisha ujenzi huu hunakatisha mkataba wake na kuangalia mkandarasi ambae atashughulikia ujenzi umalizike kwa haraka". aliongezea Katibu
Pamoja na hayo Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe.Kisare Makori alishukuru kwa ujio wa kamati hiyo ya chama kwa Wilaya ya Ubungo kwa kutembelea miradi ambayo ipo ndani ya wilaya na kuona maendeleo yake.
Nae Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo alishukuru kwa ujio wao wa kutembelea katika Miradi na kutoa changamoto inayoikumba Manispaa kwa sasa ambayo ni kutokuwepo kwa Ofisi ya kudumu ya Manispaa iliyopelekea kujenga jengo la muda ambalo linatumika kwa sasa na hiyo ni kutokana na ujenzi wa jengo la kudumu kukwamishwa na Mkandarasi ambae ni TBA kwa kuchukua muda mrefu kukamilisha jengo hilo.
Mwisho alishukuru kwa ujio wa Kamati hiyo kwa kutembelea miradi na kuona utekelezaji wake.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa