Kamati ya Siasa ya chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ubungo imefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Wilaya hiyo lengo ikiwa ni kujionea utekelezaji wa ilani ya chama hicho.
Katika ziara hiyo ambayo itafanyika kwa muda wa siku mbili kuanzia tarehe 6 hadi 7 Mei, 2021 , Kamati hiyo ikiongozwa na mwenyekiti wa chama Wilaya ndugu Lucas Mgonja. imetembelea na kukagua miradi sita yenye thamani ya zaidi ya bilioni 2.3 ikiwemo ujenzi wa mabanda ya wajasiriamali Mbezi, mradi wa maji makabe na king'azi, ujenzi wa Madarasa 3 shule ya Msingi matosa, ujenzi wa Barabara ya king'ongo hadi kimara na ujenzi wa zahanati ya Msingwa yote ikiwa inapatikana Jimbo la Kibamba
Mradi wa ujenzi wa mabanda ya wajasiriamali uliopo mbezi uliogarimu shilingi bilioni 1.6 pamoja na gharama ya fidia ya eneo.
Akizungumza baada ya kukagua miradi hiyo Mgonja alieleza Kuwa ukaguzi huo in wa kawaida ambapo chama kinawajibika kujionea utekelezaji wa ahadi mbalimbali walizoahidi wananchi kupitia ilani ya chama hi hicho.
Katika ukaguzi huo Kamati imepongeza utekelezaji wa miradi hiyo ambayo inalenga kuboresha na kusogeza huduma karibu na wananchi kama ilani ya chama hicho ilivyoahidi.
"Ujenzi wa miradi ya maji, madarasa, vituo vya kutolea huduma za afya na miundombinu ya barabara ni kutekeleza kwa vitendo ilani ya chama na ndio maana Kamati ya siasa inakagua kuona utekelezaji wake" alifafanua Mgonja.
Pamoja na pongezi hizo Kamati imeagiza kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo ili ikamilike kwa wakati na kurekebisha baadhi ya kasoro zilizobainika kwenye miradi hiyo.
Kamati hiyo itaendelea na ziara yake Kesho tarehe 7 mei, 2021 kwa jimbo la Ubungo.
Mradi wa ujenzi wa madarasa 3 shule ya msingi Matosa iliyoko kata ya Goba
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa