Leo februari 25,2022 Kamati ya Siasa Wilaya ya Ubungo imepokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa Taasisi za Serikali Wilaya ya Ubungo ikiwemo Manispaa ya Ubungo, TANESCO, DAWASA ,TRA TARURA na TANROAD katika kutatua Kero za wananchi.
Akiwasilisha kwa ufaulu taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mh Kheri James pamoja na kuelezea utekelezaji wa shughuli mbalimbali kutoka Taasisi zilizopo wilayani hapo ameeleza wajumbe juu ya uwepo wa zoezi la Anwani za makazi ambapo hadi sasa limefikia katika hatua mbalimbali ikiwemo kujenga uelewa kwa viongozi na wananchi na elimu hiyo ni endelevu.
“Zoezi hili ni muhimu na linatakiwa kutekelezwa kwa muda mfupi hivyo nawaomba kama viongozi kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu ili zoezi hili lifanikishwe kwa wakati na kwa ufanisi mkubwa” alieleza Mh. James.
Akizungumza wakati wa kikao hicho, Mwenyekiti wa Chama Mh Lucas Mgonja hicho amempongeza Mkuu wa Wilaya Mh. Kheri James kwa usimamizi mzuri wa shughuli za Maendeleo zinazolenga kutatua kero mbalimbali za wananchi ikiwemo huduma ya maji, umeme, barabara na huduma zingine ambazo zinafanya wanaubungo waipende Serikali yao.
Aidha Mh. Mgonja ameeleza kuwa mafanikio ya utekelezaji mzuri wa Ilani ya chama ni matokeo ya mahusiano mazuri kati ya chama na Serikali na uwepo wa watumishi wanaojituma katika kutekeleza majukumu yao.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa