Kamati ya Huduma za Uchumi , Afya na Elimu Manispaa ya Ubungo imefurahishwa na uwekezaji unaofanywa na kikundi cha Vijana wanaojishughilisha na shughuli za kilimo na tafiti mbalimbali ikiwa ni jitihada za kujikwamua kiuchumi na kueneza ujuzi wao kwa Vijana wengine.
Kikundi hicho kimenufaika na mkopo wa Halmashauri usio na riba kwa kupewa shilingi Milioni 30 iliyowawezesha kuandaa kitalu nyumba yaani *screen house* na kuanzisha mfumo wa umwagiliaji wa matone hali itakayoongeza uzalishaji.
Wajumbe wa Kamati hiyo wameonesha furaha hiyo baada ya kutembelea kikundi hicho wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha robo ya nne iliyoishia Juni 30, mwaka huu na kusema kuwa kikundi hicho kitumike kama shamba darasa Kwa vikundi vingine vya Vijana ambapo vitapata ujuzi wa kilimo cha kisasa na kinachozingatia utalaamu.
"Tunajivunia kuwa na kikundi chenye Vijana wasomi wanaotumia taaluma yao katika kujiajiri lakini pia kutoa ajira kwa Vijana wenzao lakini pia kuwa na uwezo wa kufanya tafiti mbalimbali zitakazoongeza tija katika uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo
Aidha, Kamati imeshauri kikundi hicho kiwezeshwe zaidi na Manispaa kwa kupatiwa mkopo mkubwa utakaowasaidia kutimiza malengo yao kwani kikundi hicho kina manufaa kwa jamii pia.
Kikundi hicho kinajihusisha na kulima mazao ya bustani, yaani nyanya, hoho na mboga mboga, kufunga samaki, inzi na nguruwe lakini pia kinajihusisha na uzalishaji wa funza Wenye kiwango kikubwa cha protini kwa ajili ya chakula cha samaki.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa