- Leo Novemba 8, 2022 kamati ya UKIMWI Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo imefanya ziara ya kutembelea Club za UKIMWI katika shule ya Msingi Makuburi Jeshini na shule ya Sekondari Yusuf Makamba na kujionea uendeshaji wa Club hizo mashuleni
- Katika Shule ya Msingi Makuburi Jeshini, Mwalimu mlezi wa club hiyo Mwalimu Cecilia Lasway Donati amesema kuwa club yao ina wanafunzi 51 na imeanzishwa mwaka 2020 na imeendelea kua ni chachu ya utoaji elimu ya kujikinga dhidi ya virusi vya UKIMWI shuleni hapo
- Kwa upande wa shule ya sekondari Yusuf Makamba mwalimu mlezi wa club hiyo mwalimu Theodosia Bilegeya amesema kuwa club yao inaendelea vizuri toka kuanzishwa kwake mwaka huu 2022 ambapo ina wanafunzi wa kidato cha kwanza na kidato cha pili tu.
- Akiongea katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya UKIMWI ambaye pia ni Naibu Meya Manispaa ya Ubungo Mhe. Yusuf Yenga amesema kuwa Club za Afya mashuleni ni muhimu sana kwenye kuongeza uelewa wa masuala ya Afya kwa wanafunzi wakiwa bado wadogo hali itakayopelekea kujua Afya zao na kuzilinda kwa kadri wanavyokuwa
- Aidha ili kuziboresha club hizo na kuratiba vizuri suala la Afya za wanafunzi, wajumbe wameshauri kuandaliwa mkakati wa kupima afya za wanafunzi wote ili kujua ukubwa wa tatizo la wanafunzi wanaoishi na Virusi vya UKIMWI ambapo itasaidia kuwalea wanafunzi hao kwa usalama zaidi kuendelea na masomo yao. Pia kamati imeshauri kuwashirikisha wazazi kwenye mchakato mzima wa kujua afya za wanafunzi katika shule zetu za Msingi na Sekondari
- Katika upande mwingine Kamati imependekeza kuandaliwa utaratibu wa chakula na matumizi mengine kwa wanafunzi ambao wanaishi na virusi vya UKIMWI ili kuendelea kuwalinda wakati wote wanapokua shuleni
- Nae Katibu wa kamati hiyo Bibi Mercy Ndekeno amewahakikishia wajumbe wa kamati hiyo kuwa mapendekezo yote yamechukuliwa na yatafanyiwa kazi kwa maslahi mapana ya Afya za wanafunzi kwenye shule za Msingi na Sekondari
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa