Wajumbe kamati ya Ukimwi Manispaa ya Ubungo tarehe 7,august,2021 wametembelea Asasi isiyo ya kiserikali ya Memorial De Porres Foundation iliyopo Kata ya Saranga Mtaa wa stop over Inayojishughulisha na magonjwa ya kifua kikuu na Ukimwi ili Kuona namna Zahanati hiyo inavyofanya kazi ya kuhudumia jamii
Akiongea wakati wa ziara hiyo mwenyekiti wa kamati ambaye pia ni Naibu Meya Manispaa ya Ubungo Hassan Mwasha ameipongeza Asasi hiyo kwa kutoa huduma kwa jamii kwa uweredi na kuwasihi kuendelea kutoa huduma kwa jamii
aidha alipokea taarifa ya asasi iliyowasilishwa na msimamizi wa asasi Salome Kafurika aliyetoa taarifa ya asasi na kueleza mambo ambayo ingehitaji kufadhiliwa kwaajili ya maendeleo na kutoa huduma kwa jamii kwa kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma
aliendelea kwa kusema kuwa asasi hiyo pia inajihusisha na utoaji wa huduma kwa jamii bure na pia ina hudumia wananchi ambao wako katika mazingira magumu kwa kuwepelekea huduma katika majumba yao
Asasi inatoa huduma ya Elimu kwa wananchi ili kuwawezesha wananchi kupata uwelewa kuhusiana na ugonjwa wa kifua kikuu na Ukimwi na jinsi ya kujikinga. aliendelea salome
Alikadhalika kamati ilipokea taarifa hiyo ya Asasi na kuahidi pale walipoona kuna changamoto watafanya juhudi ili waweze kusaidia kazi ya jamii iweze kuendelea
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa