Kamati ya kudhibiti UKIMWI Manispaa ya Ubungo leo 27.01.2023 imefanya ziara ya kutembelea kituo cha kulea wazee kilichopo Njeteni kata ya Kwembe kinachoitwa TUSHIKAMANE PAMOJA FOUNDATION chenye wazee 10 kati yao wanaume ni 6 na wanawake ni wanne
Akisoma taarifa ya kituo Afisa ustawi Hellen Samwel amesema kuwa wazee wanaochukuliwa ni waliofika miaka 60 na kuendelea na kituo hicho kinauwezo wa kuhifadhi wazee 24 ambapo mpaka sasa wako 10
Aidha, Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Naibu Meya Manispaa ya Ubungo Mhe. Yusuph Yenga amewapongeza viongozi waliojitolea katika foundation hiyo kuendelea na moyo huo huo wa kuwalea wazee hao
Yenga aliendelea kwa kuwaasa wajumbe kuhakikisha wanatembelea wahitaji hao kwa kuwapelekea mahitaji kadri mtu atakavyo barikiwa
Aliendelea kwa kusema kuwa Kama Halmashauri tutaendelea kuhakikisha wazee hao wanapata mahitaji yao kwa kushirikiana na maafisa ustawi
Wazee hawa wanapendeza na wanaonekana wanatunzwa vizuri. Alieleza hayo Yenga
Wajumbe wa kamati waliwashukuru walezi wa Kituo hicho na kuwapongeza na kuwaomba kuendelea kuwajali wazee hao
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa