- Leo Disemba 07, 2022 Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri James pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Ubungo wamefanya ziara ya kutembelea miradi ya ujenzi wa madarasa 81 unaoendelea katika shule 10 za Manispaa ya Ubungo. Ujenzi wa madarasa hayo unatokana na fedha Bilioni 1.62 ambazo zililetwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwaajili ya kuandaa mazingira mazuri ya kusoma kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2023
- Katika ziara hiyo ambayo ilianzia shule ya sekondari Kiluvya na kumalizia shule ya Sekondari Temboni Gvt, DC Kheri ameridhishwa kwa kiasi na kasi ya ujenzi wa madarasa hayo ambapo baadhi ya shule bado kasi ya ujenzi wake haujaridhisha ikiwemo shule ya sekondari Urafiki na shule ya Sekondari Makamba ambapo ametoa maelekezo ya kuanza kufanya kazi kwa masaa 24 ili kufikia muda uliopangwa wa kukabidhi madarasa hayo ifikapo Disemba 15
- Aidha katika ziara hiyo DC Kheri amesisitiza suala la ushirikishwaji wa Wananchi kwenye vikao vya maamuzi ili kuleta uwazi wa namna fedha za miradi hiyo zinavotumika. "Ushirikishwaji wa wananchi kwenye miradi hii ya maendeleo ni muhimu kwa wananchi kufahamu kila hatua ya ukamilishwaji wa miradi hiyo ili kuleta uwazi na kuhakikisha miradi inazingatia thamani ya fedha" alisema
- Sambamba na hilo DC Kheri amewasisitiza wakuu wa shule zote kumi wanaosimamia miradi hiyo kuhakikisha kuwa miradi hiyo inakamilika kwa asilimia mia moja pamoja na madawati kwa kila darasa
- Katika kuhakikisha mazingira yanakua mazuri ya shule hizo, Kamati imeshauri upandaji wa miti ya kutosha kwaajili ya kuboresha mandhari pamoja na muonekano wa shule hizo. Pia DC Kheri amekabidhi kila mradi kwa mjumbe mmoja wa Kamati ya Ulinzi na Usalama (KUU) kwaajili ya kufuatilia pamoja na kuja kukabidhiwa itakapofika Disemba 15
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa