Kamati ya Ulinzi na Usalama wa mtoto Wilaya ya Ubungo yapewa semina kuhusu ugonjwa wa korona na muwezeshaji ambaye ni Mtaalamu wa Magonjwa ya Mlipuko Dk.Baraka Chaula katika ukumbi uliopo katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya Luguruni.
Wawezeshaji wengine waliohudhulia ni Dk.Mariana Makuu ambaye ni mwenyekiti wa Taswo(Tanzania Association of Social Workers) Taifa na Digna Nsanya ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii Mwandamizi Wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Pamoja na Afisa Ustawi wa Wilaya ya Ubungo Zainabu Masilamba
Lengo la semina ni kuelimisha wajumbe jinsi ya kujikinga na maambulizi ya korona na namna wajumbe wakamati wanaweza kuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu kwa watoto walio katika jamii na wananchi waliowazunguka kuhusiana na ugonjwa wa korona na kusimamia ulinzi wa watoto na wanawake katika jamii.
"Hali ya korona kwa nchi yetu kwa sasa idadi ya wagonjwa wamefikia 20 kama ilivyoelezwa na Idara ya Afya na tuchukue tahadhali kupambana na ugonjwa huu mkawe wahamasishaji wazuri kwa jamii inayotuzunguka. alisema hayo Dk.Baraka Chaula
Aidha nitoe ufafanuzi maambukizi haya asilimia 95% ni kwanjia ya maji maji ya moja kwa moja kutoka kwa mgonjwa na asilimia 4% ni kwanjia ya kushika vifaa ambavyo vilishikwa na muathirika wa ugonjwa huo(mf.simu,peni n.k)
Niwaombe mkawe mabalozi mkaelimishe jamii na pia tuzingatie na kuhakikisha tunafunika mdomo wakati wa kukohoa,tuepukane na mikusanyiko ya watu,na tunawe mikono na sabuni kwa maji safi yanayotitirika. aliongezea Dk.Baraka
Mwisho mwakilishi wa Mkurugenzi Fortunata Shija aliwashukuru wawezeshaji kwa ujio wao na elimu waliyoitoa kwa wajumbe wa kamati.
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa