Kamati ya ULINZI na USALAMA Wilaya ya Ubungo Leo tarehe 22,disemba,2021 imeendelea kufanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya ujenzi wa madarasa katika Kata ya Goba kujionea utekelezaji wa ujenzi wa madarasa inayotekelezwa katika shule tano zilizopo Katika Kata hiyo
Ukaguzi huo ni mwendelezo wa ziara iliyofanyika tarehe 17.12.2021ambapo
Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mheshimiwa Kheri James amepongeza hatua ya ujenzi wa miradi ulipofika na kutaka Kasi iongezeke ili madarasa hayo yawe yamekamilika na kuweza kukabidhiwa pamoja na madawati ifikapo tarehe 30.12.2021 bila yakuwa na changamoto yoyote
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ni miongoni mwa Halmashauri zilizopokea fedha za ujenzi wa madarasa bilioni 3.02 kwaajili ya ujenzi wa madarasa 151 kwa shule 21 zilizotolewa kutoka Katika mgao wa fedha kwaajili ya Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya Uviko-19
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa