Kamati ya Ulinzi wa wanamke na watoto Manispaa ya Ubungo limekubaliana kuwachukulia hatua wahusika wa unyanyasaji wa watoto wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia Katika mazingira mbalimbali ikiwemo mashuleni ,mitaani na majumbani ikiwa ni Mkakati wa kutokomeza matukio ya unyanyasaji
Akiongea wakati wa kikao hicho kilichofanyika tarehe 26.10.2021 Zainabu Masilamba alisema kuwa kamati itatembelea na kutoa elimu kuhusu unyanyasaji wa kijinsia kwa wanafunzi na walimu
Aidha kamati imependekeza uanzishwaji wa clabu za kupinga ukatili wa kijinsia katika Shule zote za Msingi na sekondari ili kuwajengea uwelewa juu ya maswala hayo na kupunguza matendo ya unyanyasaji
Bi.zainabu Masilamba Katibu wa kamati hiyo alieleza kuwa kamati imefanikiwa kushughulikia ufuatilia wa kesi 25 za ukatili wa kijinsia wa watoto ikiwemo ulawiti,ubakaji na utumikishwaji ambazo zipo katika hatua mbalimbali za kisheria
Aliendelea kusema kuwa kamati imefanikiwa kuwapatia msamaha wa matibabu wazeee 1855, migogoro 249 ya matunzo ya watoto imeshughulikiwa ambapo migogoro 229 imeshughulikiwa na migogoro 20 imepelekwa mahakamani kwa hatua zaidi
Aidha, Mashauri 103 ya ndoa yameshughulikiwa Kati yao 95 yamesuluhishwa 4 yamepelekwa mahakamani na 2 yamerudishwa BAKWATA, Watoto 18 wanaume 12 na wanawake 6 wamepatiwa hifadhi ya muda Katika maeneo ambayo yapo ndani ya Manispaa ya Ubungo pamoja na kwa watu wanaoaminika
Na pia Wagonjwa 44,077 wanaume 20,039 na wanawake 24,038 wamepatiwa msamaha wa Kodi ya matibabu kwa gharama ya shilingi 146,782,484.5 zilizotolewa na Manispaa ya Ubungo kupitia vituo vyake
Kati ya vikundi 40 vilivyotarajiwa kupatiwa mikopo hiyo, vikundi 21 vya watu wenye ulemavu vimehakikiwa na kupatiwa mikopo ya vyombo vya Moto,
Na kufanikiwa maombi 5 ya malezi ya kambo yalipokelewa na kufikishwa kwa kamishna wa ustawi wa jamii
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa