Mkuu wa wilaya ya ubungo Mhe Kheri James amewataka wenyeviti na watendaji kusimamia na kutekeleza kikamilifu kampeni ya usafi, kupanga Machinga na kuhamasisha zoezi la sensa ya watu na makazi kwani ni kati ya agenda muhimu ya maendeleo.
Maelekezo hayo ameyatoa kwenye kikao kazi kilichohusisha wenyeviti na watendaji wa mitaa na kata na kueleza kuwa usafi ni agenda ya kudumu katika maeneo yao hivyo ni wajibu wao kuwasimamia wakandarasi wa usafi ili wazoe taka kwa wakati
Aidha, Mhe. James ametoa siku saba kwa watendaji wa kata za Msigani, Ubungo, Goba Manzese na Kimara kuhakikisha maeneo yao yanakuwa safi na kupanga machinga na kushindwa kufanya hivyo watachukuliwa hatua
Pia, amewataka wenyeviti na watendaji hao kuhakikisha wanahamasisha wananchi kushiriki kwenye zoezi la Sensa ya watu na makazi litakalofanyika agosti 23, 2022 nchi nzima
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa