- Mapema leo Novemba 26, 2022 Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Kheri James ameongoza zoezi la kufanya usafi wa pamoja kata ya Mbezi eneo la Round about ya kwenda Goba
- Zoezi hilo ni muendelezo wa kampeni ya usafi ambayo hufanyika kila jumamosi ya mwisho wa mwezi ambapo usafi mkubwa hufanyika maeneo yote na huazimishwa kiwilaya katika eneo moja
- Akizungumza baada ya kukamilika kwa zoezi hilo James ameendelea kuwasisitiza wananchi waliohudhuria usafi huo pamoja na wananchi wa Ubungo kwa ujumla kuendelea kutunza mazingira ili kujiepusha na magonjwa ya mlipuko lakini pia kuweka mji wetu kuwa safi na salama wakati wote
- Aidha James amewakumbusha wananchi hao kuwa ni marufuku kufanya biashara katika maeneo yote yaliyokatazwa ikiwemo pembezoni mwa barabara, chini ya madaraja na juu ya mitaro
Luguruni Area, Morogoro Road
Sanduku la Posta: P. 0. BOX 55068 Dar es Salaam
Telephone: +255 22 2926341
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: md@ubungomc.go.tz
Hakimiliki@2017 Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.Haki zote zimehifadhiwa